Hatma ya Mdee na wenzake Julai 6

0
207

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa maombi ya Mbunge wa viti maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Halima Mdee na wenzake 18 kuomba kibali cha mahakama kufanya mapitio ya kimahakama kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Halima Mdee na wenzake wamewasilisha ombi hilo wakiwa na hoja tano za kisheria ikiwemo, kufungua maombi hayo ndani ya muda wa kisheria na kuonesha maslahi yao mapana kwa Chadema na kama Wabunge wametafuta haki zao ndani ya chama hicho hadi ngazi ya juu.

Akiwasilisha hoja hizo, mmoja wa mawakili wa wabunge hao Ipilinga Panya amedai waliopeleka kuwa waliopeleka maombi wote kumi na sita wanamaslahi katika jambo hilo kwani wamekuwa waathirika wa maamuzi ya Bodi ya Wadhamini ya chama hicho kupitia uamuzi wa Baraza kuu la CHADEMA lililofanyika Mei11 mwaka huu na kufukuzwa uanachama.

Pia amedai kuwa waliopeleka maombi wote ni Wabunge wa viti maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa na Bodi ya Chama hicho mwaka 2020/2025 hivyo maamuzi ya kuwafukuza uanachama bila kufuata utaratibu wa kuwasikiliza kunagusa maslahi yao binafsi kama wanachama wa chama cha siasa na wabunge wa Bunge la Tanzania.

Wakili mwingine wa wabunge hao EBSON KILATU amedai kitendo cha baraza hilo kuwafukuza uanachama hawakuzingatia haki wakati wa utoaji maamuzi hayo.

Akijibu hoja hizo kwa niaba ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA Wakili Peter Kibatala amedai hawapingi hoja ya wabunge hao kuwa na maslahi mapana ila kigezo cha mgogoro huo kuwepo Ushahidi mahakamani ili ichunguze huo Ushahidi wao na mahakama ijiridhishe na kutoa uamuzi.

Amedai mahakama hiyo haiwezi kuwapa nafuu ianazoomba walioleta maombi kwa sababu wamewasilisha maombi hayo nje ya muda.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Julai 6 mwaka huu itakapotolewa uamuzi.