Bweni lateketea Bwiru Boys

0
108

Bweni la shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru iliyopo wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza lililokuwa likitumiwa na wanafunzi 70, limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo wakati wanafunzi wakiwa madarasani wakijisomea.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, serikali itahakikisha wanafunzi ambao vifaa vyao vimeteketea kwa moto wanapatiwa vifaa vingine ili waendelee na masomo.