Kamisaa Makinda : Watanzania wote kuhesabiwa

0
94

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kutowaficha watoto wenye ulemavu wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi, ili kutoa haki kwa kila mtanzania kuhesabiwa.

Wito huo umetolewa mkoani Dar es Salaam na Kamisaa wa sensa mwaka 2022 Anne Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kongamano la viongozi wa dini kuhusu sensa ya watu na makazi.

Amesema siku ya kuhesabiwa kila mtu atakayekuwepo nchini atatakiwa kuhesabiwa hata kama sio mtanzania, hivyo viongozi wa dini waendelee kuwakumbusha waumini wao kuhusu jambo hilo.

Amesema sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu itafanyika kidigitali zaidi, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu utekelezwaji wa zoezi hilo.

Mama Makinda amesema sensa ya watu na makazi imetanguliwa na zoezi la uwekaji wa anwani za makazi, na kwamba mambo hayo yote mawili yataisaidia serikali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo.