Kufuatia majadiliano na wadau mbalimbali, michango ya wabunge wakati wakijadili bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 pamoja na maoni ya Kamati ya Bunge ya Bajeti, Serikali imefanya marekebisho mbalimbali ya hatua za mapato zilizowasilishwa kupitia hotuba ya bajeti.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ameyasema hayo wakati akiwasilisha muswada wa sheria ya Fedha wa mwaka 2022 bungeni jijini Dodoma .
“Serikali inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, Sura ya 197 kwenye vifungu vya 35(2) na 36(1) ili kuongeza kiwango cha ukomo wa Serikali kukopa kutoka Benki Kuu. Lengo la marekebisho haya ni kuiwezesha Serikali kutekeleza Bajeti zake kwa ufanisi hususan kwenye kutekeleza miradi ya maendeleo.” amesema Dkt. Nchemba