Tanzania kushiriki mkutano wa uhifadhi bahari

0
176

Mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhifadhi wa bahari na rasilimali zake unaanza hii leo huko Lisbon nchini Ureno.

Miongoni mwa malengo ya mkutano huo ni kuhamasisha juhudi za mataifa katika kufanikisha utekelezaji wa lengo la 14 la maendeleo endelevu na mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.

Makamu wa Rais wa Dkt. Philip Mpango ambaye tayari yupo nchini Ureno, anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo utakaofikia tamati Julai mosi mwaka huu.

Mkutano huo wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhifadhi wa bahari na rasilimali zake unararajiwa
kuhudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wadau wa mazingira pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali duniani.