Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinaendelea na maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi na wawekezaji.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wawekezaji kutoka TIC Anna Lyimo amewakaribisha wananchi na wawekezaji kutembelea ofisi za kituo hicho ili kupata elimu juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na tafiti mbalimbali zinazoibua fursa za uwekezaji nchini.
“Kituo kimedhamiria kuelimisha juu ya maboresho ya teknolojia katika utoaji wa huduma chini ya Kituo cha Mahala Pamoja namna kinavyorahisisha upatikanaji wa leseni, vibali, na usajili wa mradi.”ameongeza Lyimo