Maombi ya kina Mdee yatupwa

0
233

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Halima Mdee  na wenzake kutokana na kasoro katika jina la mjibu maombi wa kwanza.

Halima ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Wanawake la chama cha Democrasia na Maendelea – CHADEMA (BAWACHA) na wenzake waliomba kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama wa CHADEMA katika mahakama hiyo.

Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

CHADEMA iliweka pingamizi ikiiomba Mahakama Kuu isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria.