Wabunge kupiga kura kulivunja bunge

0
185

Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett amekabidhi madaraka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Yair Lapid hadi hapo wabunge watakapopiga kura ya kulivunja bunge la nchi hiyo, kutokana na mzozo uliojitokeza katika serikali ya mseto ya nchi hiyo.

Mzozo huo uliibuka kutokana na kutofautiana maamuzi ndani ya serikali, hatua ambayo ilisababisha Baraza la Mawaziri kushindwa kupitisha muswada wa kuwalinda walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina.

Waziri Mkuu Naftali Bennett alilazimika kuunda serikali ya mseto baada ya chama chake kushindwa kupata idadi kubwa ya wabunge.

Mtangulizi wa Bennett, Benjamin Netanyahu alilazimika kujiuzulu baada ya wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, hatua ambayo inaifanya Israel kuwa na rekodi ya kuwaondoa madarakani mawaziri wakuu kutokana na sababu mbalimbali.