M23 wataka mazungumzo na DRC

0
138

Waasi wa kundi la M23 wamesema wako tayari kurejea katika mazungumzo ya amani na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), huku mgogoro kati ya pande hizo mbili ukizidi kuongezeka.

Waasi hao ambao wameiteka baadhi ya miji katika eneo la mashariki mwa DRC wametangaza uamuzi huo huku juhudi za kutatua mgogoro huo ambao pia umeihusisha Rwanda zikiendelea.

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kupeleka kikosi cha kulinda amani huko DRC, kikosi kitakachokuwa na jukumu la kupambana na makundi ya waasi nchini humo.