NYANI WAPOKONYA MTOTO, WATOKOMEA NAYE PORINI

0
132

Kundi la nyani kutoka hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, limevamia nyumba ya Shayima Faya mwenye umri wa miaka 20 na kumpokonya mtoto mchanga wakati akimnyonyesha na kutokomea naye porini ambapo baadaye mtoto huyo alifariki dunia.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea tarehe 18 mwezi huu katika kijiji Mwamgongo.

Amesema baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele  kuomba msaada na majirani walijitokeza kudhibiti wanyama hao ambao walimtupa mtoto huyo chini akiwa tayari amejeruhiwa.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Kigoma, mtoto huo alijeruhiwa kichwani, usoni na mguu wa kushoto na baada ya kufikishwa kituo cha afya Mwamgongo alikuwa tayari amefariki dunia.