Baraka Shamte avuliwa rasmi uanachama CCM

0
189

Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Zanzibar, imeridhia na kuunga mkono mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mjini ya kumfukuza uanachama Baraka Shamte ambaye ni Mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao amesema Kikao hicho kilichokaa tarehe 14 mwezi huu pamoja na mambo mengine kwa kauli moja kimeunga mkono pendekezo la kufukuzwa uanachama kada huyo.

Mwanasiasa huyo anadaiwa kukashifu hadharani madaraka ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Uamuzi huo umekuja baada ya Shamte kuzungumza mambo kadhaa na video yake kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.