Wakazi wa Ngorongoro waanza kuhamia Msomera

0
128

Kundi la kwanza la kaya 20 za wakazi wa kata ya Ngorongoro waliokubali kahama kwa hiari ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha, limeondoka kuelekea katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga ambapo serikali imejenga nyumba kwa ajili ya wakazi hao.

kundi hilo ni sehemu ya kaya 290 za wakazi wa Ngorongoro ambao wamejiandikisha kahama kwa hiari ili kupisha uhifadhi katika eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Shauku ya muda mrefu ya wakazi wa Ngorongoro kuhama eneo hilo imetimia baada ya kundi la kwanza kukabidhiwa stakabadhi ya malipo yao ya fidia na kuanza safari ya kwenda wilayani Handeni.

Baadhi ya wakazi hao wamesema safari yao ya kuanza maisha mapya imekuwa rahisi kutokana na namna serikali ilivyowaandalia makazi mapya pamoja na fidia waliyolipwa.

Kuanza kuhama kwa wananchi hao wa Ngorongoro kunafungua milango kwa wakazi wengine waliojiandikisha kuhama kwa hiari kuanza safari ya Msomera ambako serikali imejenga nyumba zaidi ya mia moja na nyingine zikiendelea kujengwa.