SAILI ZIFANYIKE KISWAHILI

0
136

“Kwa nini usaili wa mtoto wa kitanzania anapotafuta kazi unafanyika kwa lugha ya Kingereza?, yani afisa kilimo, afisa mifugo, mtumishi wa serikali ana kazi ya kuhudumia watanzania tunapima akili zake kwa kupima kiingereza chake kwa ajili ya nini?.

Napendekeza saili zote zifanyike kwa Kiswahili na kumbi zote za mikutano na ofisi za serikali ziwe na vifaa vya kutafsiria lugha za kigeni na watafsiri ili tuweze kuienzi lugha yetu ya Taifa.”Dkt. Mwigulu Nchemba