Shabiki mlemavu wa Man U apanda Kilimanjaro

0
224

Klabu ya Manchester United ya Uingereza imempongeza shabiki wake Martin Hibbert (45) ambaye amepanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya msaada.

Hibbert alipooza kuanzia kiunoni kushuka chini kufuatia shambulizi la mwaka 2017 kwenye uwanja wa jiji hilo.

Licha ya kuambiwa kwamba hatoweza kutembea tena baada ya kupata madhara kwenye uti wa mgongo, alidhamiria kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wenye matatizo ya uti wa mgongo katika taasisi iliyompa tumaini na kujiamini pamoja na kumsaidia mazoezi.

Mlima Mrefu zaidi Afrika ndio uliochaguliwa kama njia ya kuchangisha fedha hizo, nia ambayo ameifanyia kazi kwa miaka miwili.

Akitumia kiti maalum cha magurudumu, pamoja na usaidizi wa watu wengine, ameweka rekodi ya kuwa mtu wa pili ambaye sehemu yake ya chini ya mwili haifanyi kazi kufika kilele cha mlima huo.

Akifanya mahojiano baada ya safari hiyo ameishauri jamii kutowaona wenye ulemavu hawana uwezo, lakini ukweli ni kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa wakipata usadizi kutoka kwa watu sahihi.