Man U yapigania ubingwa

0
1035

Kocha wa muda wa timu ya Manchester United, – Ole Gunner  Solskjaer amesema kuwa timu yake haipiganii kumaliza ligi ikiwa kwenye Top 4 bali inapigania ubingwa.

Kwa sasa Manchester United ni ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England na bado iko kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya na kombe la FA ambapo watapambana na Chelsea kwenye mzunguko wa tano.

Ole Gunnar Solskjaer aliyechezea Manchester United kwa muda wa  miaka  11 amesema kuwa, siku zote timu hiyo ni ya kuwania mataji na sio ya kupigania kuingia kwenye Top 4.

Jeuri ya kocha huyo inakuja baada ya kushinda michezo yake yote sita aliyoiongoza timu hiyo tangu achukue jukumu hilo toka kwa Jose Mourihno.

Pamoja na maneno hayo ya kujiamini ya Ole Gunnar, lakini timu yake iko nyuma kwa pointi 16 dhidi ya vinara Liverpool, na ina tofauti ya pointi nne tu kutinga kwenye Top 4.