Dar es Salaam yaongoza kwa matukio ya moto

0
114

Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini ameutaja mkoa wa Dar es Salaam kuwa ndio unaoongoza kwa matukio ya moto nchini.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Temeke, Dorothy Kilave, Naibu Waziri Sagini amesema serikali imejiridhisha kuwa matukio hayo yanatokana na uzembe na mengine ni miundombinu mibovu.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/ 2023 magari matatu yanayotengenezwa na kiwanda cha Nyumbu yatagawiwa kwenye mikoa yenye matukio mengi ya moto ukiwemo mkoa wa Dar es salaam.

“Hata hivyo mwaka ujao tunayo bajeti ya zaidi ya Euro milioni 4.9 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya magari na maeneo yote yenye changamoto yatagawiwa vifaa hivyo.” amesema Naibu Waziri Sagini