Dkt. Bashiru: Lishe bado tatizo Kagera

0
182

Mbunge wa Kuteuliwa Dkt. Bashiru Ally amemwambia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mkoa wa Kagera bado una tatizo kubwa la lishe na hivyo watu wengi wana utapiamlo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa Rais na wananchi wa mkoa wa Kagera, Dkt. Bashiru amesema mkoa huo umekuwa na tatizo la utapiamlo kwa watu wake linalosababishwa kwa kiasi kikubwa na lishe duni.

Dkt. Bashiru amemkumbusha Rais Samia kuhusu ajenda yake ya lishe ambayo amekuwa akiizungumza na kuisimamia na kumuomba aendelee nayo ili kunusuru wananchi wanaokabiliwa na utapiamlo.

“Mhe. Rais naomba nikukumbushe kuhusu ajenda yako ya lishe ambayo nimekuwa nikikusikia ukiisema mara kwa mara na hapa mkoani Kagera hilo limekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi wetu” amesema Dkt. Bashiru