Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na watendaji waandamizi wa benki ya Equity wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Afrika Mashariki na Kati Dkt. James Mwangi ofisi kwake Mlimwa jijini Dodoma
Katika Mazungumzo hayo watendaji hao wamewasilisha mpango wa Equity Group Holdings ujulikanao kama ‘African Recovery and Reliance Plan’ wenye lengo la kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania na ustawi wa watu wake.
Waziri Mkuu amewaahidi kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano katika kutekeleza malengo yao ya kiuchumi na kijamii.
Pia amewataka wafungue matawi mengi zaidi hapa nchini ili yaweze kusambaa hadi kwenye ngazi ya wilaya na kutoa huduma za kifedha kwa watu wengi zaidi.