Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya UVIKO – 19 kwa kuendelea kuchanja na kujilinda.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la Kyaka wilayani Misenyi mkoani Kagera, Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi kuendelea kuchanja na kujilinga na maambukizi ya ugonjwa huo ambao bado upo.
“Nawasihi wananchi tuendelee kuchanja dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 kwani ugonjwa huu bado upo na kama tukichanja basi maradhi hayo yakitupata tunakuwa imara.” amesema Rais Samia
“Nikiangalia hapa wengi hamjavaa hata barakoa, nawasihi mchukue tahadhari kwani maradhi haya bado yapo ila kwa sasa yametupa likizo tu.”ameongeza Rais
Kwa mujibu wa wizara ya Afya, kwa sasa Tanzania ina wagonjwa wapya 161 wa UVIKO – 19.