Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti ametoa muda wa siku saba kwa chama Kikuu cha Ushirika cha Mtwara, Masasi na Nanyumbu (MAMCU) kumaliza kugawa pembejeo kwa wakulima.
Brigedia Jenerali Gaguti ametoa muda huo wakati akizungumza na wakulima wa korosho wa vijiji vya Mtiniko na Nitekela vilivyopo katika halmashauri ya mji wa Nanyamba wilaya ya Mtwara.
Amesema serikali imetoa pembejeo hizo bure ili kuwawezesha wakulima wa korosho kuongeza uzalishaji, hivyo hakuna sababu ya zoezi la ugawaji kufanyika polepole, jambo linaloweza kuathiri uzalishaji wa zao hilo.