Kombe Jipya Ligi Kuu

0
141

Bodi ya Ligi kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu Almas Kassongo, leo imetambulisha kombe jipya atakalokabidhiwa bingwa wa msimu huu katika Ligi Kuu ya NBC.

Bodi hiyo pia imetaja kitita cha shilingi bilioni 1.8 kama zawadi na bonasi kwenye ligi msimu huu, huku bingwa akitengewa shilingi milioni 100 kutoka NBC na shilingi milioni 500 kutoka Azam.