Mmiliki wa salfa ‘feki’ atakiwa kujisalimisha

0
115

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti ametoa muda wa saa 48 kwa mmiliki wa kiuatilifu cha salfa ya unga chapa Makonde kujisalimisha kwa madai ya kusambaza kwa wakulima kiuatilifu bandia.

Brigedia Jenerali Gaguti ametoa muda huo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari na kuongeza kuwa tayari watu saba wanashikiliwa na polisi kwa kukutwa na zaidi ya mifuko elfu mbili ya kiuatilifu hicho katika wilaya za Tandahimba na Newala mkoani Mtwara.

Amesema watu wanne ambao ni wafanyabishara wamekamatwa wilayani Newala wakidaiwa kuwa na mifuko elfu moja na mia sita na wengine watatu katika wilaya ya Tandahimba wakiwa na mifuko mia tano ya kiuatilifu hicho.