Tanzania na Marekani kuimarisha ushirikiano sekta ya elimu

0
181

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Dkt. Donald Wright ambapo wamekubaliana kuendeleza ushirikiano katika sekta ya elimu.

Baadhi ya maeneo ya kipaumbele katika ushirikiano huo ni kuendeleza sayansi, teknolojia na elimu ya tiba ambapo kutukuwa na fursa za wanafunzi kwenda kusoma nchini Marekani katika maeneo hayo.

Profesa Mkenda amemueleza Balozi Wright kuwa kwa sasa kipaumbele kwenye sekta ya elimu nchini ni kufanya mageuzi ya elimu ili elimu inayotolewa iweze kutoa ujuzi bila kuathiri ubora.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Dkt. Donald Wright amesema nchi hiyo inafurahi kuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu.