Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaofanyika Geneva, Uswisi.
Mapema hii leo, Waziri Ndalichako ameshiriki kikao cha kundi la Afrika ambapo ametoa salamu za Tanzania na kuwaalika nchi wanachama kutoka Afrika na Duniani kote kuitembelea Tanzania ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii.