Kampeni uchaguzi mkuu Kenya zapamba moto

0
143

Mgombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu nchini Kenya kupitia muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, amezindua ilani ya uchaguzi ambayo pamoja na mambo mengine inaeleza namna atakavyopambana na rushwa, kuimarisha uchumi na usalama.

Akizindua ilani hiyo ikiwa ni sehemu ya kampeni za uchaguzi mkuu katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Odinga amewaomba wananchi wa Kenya kumwamini na kumpa ridhaa ya kuongoza nchi baada ya kuidhinishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (IEBC) kugombea nafasi hiyo.

Kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha urais na nafasi nyingine ikiwemo ya ugavana kinazidi kupamba moto nchini Kenya baada ya kuzinduliwa rasmi kwa kampeni za uchaguzi huo mkuu.

Raila Odinga anachuana vikali na Makamu wa Rais William Ruto ambaye anagombea urais kupitia muungano wa Kwanza Alliance.