TET na Siloam kusaidia wanafunzi wasioona

0
108

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo Juni 6,2022 imefanya mazungumzo na Shirika la Siloam Center for the Blind la nchini Korea katika ofisi za TET zilizopo Jijini Dar es salaam, Mazungumzo ambayo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya TET na shirika hilo wenye lengo la kushirikiana katika kuandaa vitabu vya Breli kwa ajili ya wanafunzi wasiona wa ngazi zote za elimu nchini.

Katika Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Siloam Center for the Blind Dong ic Choi ameahidi kuwa kwa mwaka huu wa fedha shirika lake litachapa vitabu katika maandishi ya Breli kwa vitabu vyote vya Kiada vya Ngazi ya Elimu ya Sekondari vitakavyoandaliwa na TET.

Katika ushirikiano huu Siloam watazalisha vitabu Nchini Korea kwa kutumia technolojia ya kisasa na kuvisafirisha mpaka Tanzania, ambapo TET itafanya jukumu la kuvitoa Bandarini na kuvisambaza katika shule husika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania Siloam ameshukuru na kuahidi kutimiza majukumu yao kwa wakati ili kuhakikisha wanafunzi wasioona wanapata haki yao ya msingi ya kupata vitabu vya kujifunzia kwa wakati.

Vitabu hivyo hugawiwa kwa uwiano wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja.