Tanzania yatinga fainali za kombe la Dunia

0
165

Timu ya Taifa wa wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imefuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwezi Agosti mwaka huu nchini India.

Timu hiyo imefuzu kwa fainali hizo baada ya hoo leo kuifunga timu ya Taifa ya wanawake ya Cameroon bao moja kwa bila katika mchezo uliopigwa katika Dimba la Amaan, Zanzibar.

Kwa matokeo hayo Serengeti Girls inafuzu kwa jumla ya mabao matano kwa moja baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.