Tido Mhando aachiwa huru

0
1478

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania -TBC, Tido Mhando ameachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia dhidi ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara ya zaidi ya Shilingi Miloni Mia Nane.

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Wilbard Mashauri amesema hakuna ushahidi unaoonyesha mikataba hiyo kusainiwa na Mwanasheria Mkuu wa mwanasheria mkuu wizara husika wala mjumbe yeyote wa Bodi ya TBC.

Hakimu Mashauri amesema mikataba ya serikali ni lazima ihusishe ofisi ya mwanasheria mkuu na taasisi zinazohusika na kwa kesi ya TBC mikataba hiyo haikukidhi vigezo vya kuwa   mikataba na hakuna ushahidi unaonyesha mwendelezo wa kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Channel Two Jijini London