Shaka ataka matumizi mazuri ya chakula Mtwara

0
172

Watanzania wametafkiwa kutumia vizuri chakula ili kukabiliana na tishio la njaa linaloonyemelea Afrika.

Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ametoa wito huo kwenye kwa nyakati tofauti wakati akizungunza na wananchi wa Wilaya ya Tandahimba na halmashauri ya Nanyamba mkoa wa Mtwara ambako yuko kwenye ziara ya siku nne.

“Ndugu zangu shirika la chakula duniani limetangaza tahadhari ya hali ya chakula duniani, kwa hiyo naomba tuweke akiba ya chakula” amesema Shaka na kuongeza

“Nchi kadhaa zimetangaza hali ya hatari hao wanaoshughulika na chakula duniani(WFP) wanasema watu zaidi ya milioni 80 Afrika wako kwenye hatari hiyo”

Amesema vita vya Ukraine vimechangia hali hiyo.” Mnasikia kwenye vyombo vya habari vita huko Ukraine vimesababisha upungufu wa ngano kwa sababu asilimia takriban 40 ya ngano inatoka huko”