Wakandarasi na Wahandisi wampongeza Rais

0
138

Wakandarasi na Wahandisi wa Miundombinu nchini, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupokea tuzo ya Mjenzi Mahiri (Babacar Ndiaye Trophy 2022) nchini Ghan

Akitoa Pongezi hizo kwa niaba ya wakandarasi na wahandisi katika Kongamano lililofanyika jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya Rais Samia amefanya makubwa kwenye sekta ya miundombinu hivyo ni vema kupongezwa kwa juhudi zake.

“Barabara zenye urefu zaidi ya Kilomita 2500 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami katika awamu hii ya sita” – amesema Naibu waziri Kasekenya

Aidha Naibu Waziri Godfrey Kasekenya amesisitiza kuwa malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwapa kipaumbele wakandarasi wa ndani wanaoweza kufanya kazi na waaminifu.

“Rais hatotoa kazi ili mradi tu wewe ni mtanzania ila kazi zitatolewa kwa mwenye uwezo wa kufanya kazi na nina amini uwezo huo tunao, unganeni tunaamini barabara ya kilomita 100 achukue mkandarasi Mtanzania” amesema Naibu waziri Kasekenya

Naye Mweyekiti wa Wakandarasi na Wahandisi wazawa Tanzania Thobias Kyando amesema ni muhimu sekta za Umma kushirikiana na sekta binafsi sababu Rais Samia ameonyesha kuziamini sekta binafsi sababu ndio injini ya maendeleo nchini.

“Ni ukweli usiopingika kwamba makandarasi wa ndani tumenufaika chini ya uongozi wa awamu ya sita, takwimu za bodi ya makandarasi zinaonyesha kati ya miradi yenye thamani ya Trioni 4.9 zilizosajiliwa mwaka 2021/2022 miradi iliyofanywa na makandarasi wa ndani ni miradi yenye thamani ya Trioni 2.8 sawa na asilimia 57 na miradi iliyofanywa na makandarasi wa nje ni miradi yenye thamni ya Trioni 2.1 sawa na asilimia 43″- amesema Kyando