Muuguzi anaswa na kilo 174 za heroine

0
139

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imemkamata Salum Shaban ambaye ni muuguzi msaidizi mkazi wa Tabata Relini mkoani Dar es Salaam akiwa na kilo 174.77 za dawa za kulevya aina ya Heroine.

Kamishna Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya amesema hayo mkoani Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mambo mbalimbali yaliyofanywa na mamlaka hiyo kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu.

“Bwana Salum Shaban ambaye ni nesi msaidizi katika zahanati moja huko Kariakoo alikamatwa Mei 12, 2022 nyumbani kwake huko Tabata Relini akiwa ameweka kilo 174.77 za dawa za kulevya zikiwa juu ya kitanda chake, huku yeye akiwa amelala chini.” amesema Kamishna Jenerali huyo wa DCEA