Simba yamtupia vilago Pablo

0
136

Timu ya Simba SC ya Dar es Salaam imefikia uamuzi wa kumtupia vilago kocha wa timu hiyo Pablo Franco Martin na kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes.

Katika taarifa yake kwa umma, Simba imesema pande zote mbili zimekubaliana kuvunja mkataba wa makocha hao ambao walikuwa bado hawajamaliza kuitumikia timu hiyo.

Pablo na Castro wameiwezesha timu ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kufikia robo fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.