Mwendokasi Mbagala rasmi Machi 2023

0
208

Wakala wa Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umesema kuwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka kwa barabara kuanzia Mbagala kuelekea Gerezani utaanza Machi 2023.

Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu wa DART Dkt. Edwin Mhede na kuongeza kuwa wakala huo unajivunia mifumo ya ukusanyaji mapato ambapo imeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.8 hadi kufikia shilingi bilioni 3 kwa mwezi.

Amesema kuwa malengo ambayo wamejiwekea ni kuhakikisha wanakwenda kutoa huduma bora ya usafiri katika mkoa wa Dar es Salaam ambayo itachochea na uchumi kukua.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Abdallah Chaurembo ambaye ni Mbunge wa Mbagala amesema kuwa, mradi huo uko vizuri na kushauri maeneo yenye kasoro yarekebishwe.