Vibanda 250 vyateketea kwa moto Vetenari

0
203

Vibanda 250 kati ya 453 vimeteketea kwa moto baada ya soko la Vetenari lililopo Temeke mkoani Dar es Salaam kuungua moto usiku wa kuamkia hii leo, moto unaodaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme sokoni hapo.

Akizungumza baada ya kutembelela soko hilo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema serikali itachukua hatua za haraka kuhakikisha wafanyabiashara katika soko hilo wanarejea sokoni hapo na kuendelea na shughuli zao.

Amemuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuchukua hatua za haraka kushugulikia suala hilo.

Soko hilo la Vetenari limeungua moto likiwa na jumla ya wafanyabiashara 803.