Viongozi Wizara ya Michezo Watembelea Kambi Twiga Stars

0
197

Viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, wakiongozwa na Waziri Mohammed Mchengerwa , leo wametembelea kambi ya Timu ya Taifa ya Wanawake U17, Serengeti Girls, iliyopo Zanzibar, kuwatia motisha wachezaji hao kuelekea mchezo wao wa mwisho wa kufuzu kwenda Kombe la Dunia India dhidi ya Cameron.

Akizungumza katika kikao na wachezaji hao, Waziri Mchengerwa amewataka kujitambua na kutimiza majukumu yao uwanjani kama walivyofanya ugenini ambako walishinda 4-1. Amewapa ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema Rais yuko pamoja nao.

Naye Naibu Waziri wa Michezo Pauline Gekul amewataka mabinti hao kuzingatia maadili na nidhamu wakiwa kambini wakati huu wakielekea katika mechi hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, amesema Serikali imeilea timu hiyo kwa kushirikiana na TFF tangu mwanzo na timu haina changamoto zozote huku akiwasomea aya vijana hao kutoka kwenye Quran Tukufu akiwataka wawe na subra na waelekeze nia zao katika jambo moja muhimu; nalo ni kushinda mechi hiyo na kufuzu kwenda Kombe la Dunia nchini India.