Michezo itumike kujenga Afya ya Akili

0
102

Michezo imetajwa kuwa njia ya kutatua changamoto Katika Jamii kwakuwa inawaleta watu Pamoja na kwa kutumia michezo kunaifanya Akili ya Mtu kupata ahueweni kutokana na shughuli za kibinadamu za kila Siku.

Hayo yamesemwa na mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Elesia George wakati wa kufunga mafunzo ya Afya ya Akili na saiokolojia kwa maafisa ustawi wa Jamii, wahudumu wa Afya na Azaki zianazotoa huduma za Afya ya Jamii yaliyofadhiliwa na Amref na kuratibiwa na Shirika la PHEDES Tanzania

Elesia amesema Jamii inapaswa kutenga muda wa kufanya mazoezi ambayo yataisaidia jamii kuwa na Afya njema ya Akili na utulivu wa Saikolojia huku akisisitiza umuhimu wa mazoezi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa PHEDES Tanzania John Ambrose amesema michezo inasaidia kuwa na uwezo wa kufikiri sawasawa na kuchangamsha Akili pamoja na kutatua changamoto za Maisha.