Wabunge wapendekeza mafunzo ya JKT kuwa lazima

0
128

Baadhi ya wabunge wameomba mafunzo ya ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) yawe lazima na sio hiari kwa wabunge wote ambao hawajawahi kupitia mafunzo hayo,ambayo lengo ni kuwajengea uzalendo, ukakamavu na nchi iwe askari wa akiba kwa kuanzia na wabunge.

Hayo yamesemwa na mbunge wa viti Maalumu, Ester Bulaya baada ya Mwenyekiti wa Bunge Najma Giga kutanzgaza fursa kwa Wabunge ambao wanataka mafunzo hayo wajiandikishe ili kwenda mafunzo ya JKT.

Mwenyekiti Giga amesema kuwa ofisi ya bunge ilianza kutoa fursa hiyo kwa watumishi wa bunge vijana kwenda kwenye mafunzo ambayo kawaida yameshawai kufanyika kwa baadhi ya wabunge na yanafanyika katika kikosi cha Jeshi 834 Makutupora, Mkoani Dodoma kwa muda wa siku 38 kwa lengo la kujenga nidhamu ,utii, uadilifu, ukakamavu, uhodari, uvumilivu na uzalendo kwa nchi.

Pia Mbunge wa Geita vijijini Joseh Kasheku ‘Musukuma’ kufuatia tangazo hilo naye ametoa mapendekezo kwa kuomba mwongozo kwa Mwenyekiti na kusema kwa nini ni vijana tu hata wazee wapewe nafasi hiyo

“JKT ni sehemu ya kufundisha uzalendo na kwa vile hii taasisi ya bunge tunahitaji kuwa na uzalendo wa hali ya juu kwanini tunabagua wabunge vijana, kwanini tusiende wote na wabunge wazee”. alihoji Musukuma.

Mwenyekiti Najma Giga amemaliza kwa kutoa mwongozo kwa Wabunge na kusema ni tangazo hivyo atalirudisha ili Wabunge wakae na kujadili ili kuona umuhimu wakufanya mafunzo kwa vijana ambao hawajapita JKT kwa lazima au hiari.