CRDB kuwafikiria wachimbaji wadogo

0
1175

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, – Abdulmajid Nsekela amesema kuwa  kwa muda mrefu imekua ni vigumu kuwakopesha wachimbaji wa madini nchini kutokana na wachimbaji hao kutokuwa na makazi ya kudumu.

Nsekela ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati wa mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini, mkutano uliokuwa na lengo ya kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wadogo wa madini na namna ya kuzitatua changamoto hizo.

Amesema kuwa hatua ya wachimbaji hao wa madini kutokuwa na makazi ya kudumu, inawawia vigumu watendaji wa benki hiyo ya CRDB kuwafuatilia ili kuwapatia mikopo.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya CRDB, – Abdulmajid Nsekela  amesema kuwa pamoja na ugumu huo,  bado ipo nafasi ya kuzungumza na wachimbaji hao wa madini kwa lengo la kuona  namna ya kuweza kuwapatia mikopo kuanzia hivi sasa.