Ajali yaua watatu Manyara

0
112

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 26 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea wilayani Hanang’ mkoani Manyara.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajalli hiyo na kuongeza kuwa imelihusisha basi la Mohamed Classic lenye namba za usajili T643 DJP lililokuwa likitokea mkoani Arusha kwenda Kigoma na roli aina ya fuso lenye namba ‘za usajili T380 DWF lillilokuwa likitokea Singida kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro.

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni dereva wa fuso na msaidizi wake pamoja na dereva msaidizi wa basi la Mohamed Classic.