Watakiwa kufunika nyuso wakisoma habari

0
239

Watangazaji na waandishi wa habari wanawake nchini Afghanistan walilazimika kurusha matangazo wakiwa wamefunika sehemu ya nyuso zao Mei 22 mwaka huu, ikiwa ni agizo la uongozi wa Taliban.

Mmoja wa watangazaji alisema kuwa wanawake wanaofanya kazi kwenye vituo vya televisheni waligoma kutekeleza amri hiyo, lakini waajiri wao waliwalazimisha kufanya hivyo kutokana na shinikizo juu yao.

Wakiwa wamevalia hijabu na kufunika nyusi zao wanawake hao walitangaza na kuripoti habari na vipindi vingine kwenye vituo mbalimbali vya televisheni kama vile TOLOnews, Ariana TV, Shamshad TV na 1TV.

Baada ya kutwaa madaraka mwaka jana, Taliban imeendelea kutekeleza amri mbalimbali katika mtindo wa maisha ya wanawake.