Wizara ya Habari yaomba bilioni 282

0
425

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeomba shilingi bilioni 282 kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 26 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi Bilioni 255 kinaombwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Bajeri ha wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 imewasilishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye.