Waziri wa Afya azindua kampeni chanjo ya Polio

0
222

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezindua Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Matone Dhidi ya Ugonjwa wa Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Dodoma leo, Mei 18, 2022.

Akizindua kampeni hiyo Waziri Ummy ameeleza kuwa kampeni hiyo ni mwendelezo wa kampeni ya kidunia inayoendelea hivi sasa na Tanzania ni miongoni mwa nchi za Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) zinazotekeleza kampeni hii ambayo leo imezinduliwa rasmi Tanzania.

Akizungumza katika kampeni hiyo Waziri Ummy amebainisha matarajio ya Serikali kutoa chanjo kwa watoto zaidi ya milioni 10 kwa Tanzania bara na visiwani.