Barabara ya Tabora – Koga – Mpanda yawa mkombozi

0
108

Ujenzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda umeokoa maisha ya wakazi wengi wa maeneo hayo ambao awali walikuwa wakikumbwa na mafuriko kipindi cha masika, kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya uhakika.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Batilda Buriani wakati wa ufunguzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda, uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Barabara hiyo Ina urefu wa kilomita 342.9 na inaunganisha mkoa wa Tabora na ule wa Katavi.

Dkt. Buriani amesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kutakuza kipato cha wakazi wa mkoa wa Tabora ambao sasa wataweza kusafirisha bidhaa zao ikiwa ni pamoja na asali, tumbaku, pamba na karanga zinazolimwa kwa wingi mkoani humo.

Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya siku tatu ambapo anazindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wakazi wa mkoa huo.