Tanga yakabiliwa na kesi nyingi za dawa za kulevya

0
263

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesema mkoa wa Tanga unakabiliwa na changamoto ya uwepo wa kesi nyingi za dawa za kulevya pamoja na kesi za mashauri ya mirathi.

Profesa Juma ametoa kauli hiyo wilayani Pangani mkoani Tanga alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo, pamoja na watumishi wa mahakama.

Amesema Kwa sasa mahakama nchini inaendelea na utaratibu wa ujenzi wa majengo ya mahakama jumuishi awamu ya pili kwa baadhi ya mikoa.

Amesema mikoa iliyofanikiwa kujenga majengo hayo Kwa awamu ya kwanza ni ile iliyowasilisha mapema hati za maeneo ambayo hayana migogoro ya ardhi.

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma yupo mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku tano, ambapo na anatarajiwa kutembelea wilaya zote nane za mkoa huo.