Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai amewataka wazazi kukaa na familia zao katika kuwafundisha maadili mema, upendo na amani watoto wao.
Akizungumza katika siku ya familia, Kagaigai amesema wapo baadhi ya watoto hawana maadili hivyo wazazi wanatakiwa kutumia siku hii katika kuwafundisha yaliyo mema.
Kagaigai amesema ni wakati sasa wa familia pia kutumia siku ya familia kufanya tathmini ili kuangalia changamoto zinazozikabili familia na kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema majukumu ya kutafuta kipato cha kuendesha maisha yanawafanya wanakosa muda wa kukaa na familia hivyo kuchangia mmomonyoko wa maadili.
Kauli mbiu ya mwaka huu, “Dumisha Amani na Upendo kwa Familia imara, Tujitokeze kuhesabiwa”