Maofisa habari wapewa somo

0
161

Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Chacha Rioba amewataka maafisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini kulinda na kuthamini utamaduni pamoja na kutanguliza mbele uzalendo Kwa maslahi mapana ya taifa.

Dkt. Rioba ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati alipokua akiwasilisha mada kwa maafisa habari mawasiliano na uhusiano serikalini kutoka taasisi na wizara mbalimbali za serikali.

Amesema ni vema kila moja akatimiza wajibu wake katika eneo lake ili kudumisha sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Aidha amewataka maofisa hao kutathimini mambo Kwa kina huku wakizingatia maadili na kuonyesha uzalendo katika kutimiza majukumu yao.