Serikali yasisitiza hatua kali kwa wanaofanya ukatili

0
154

Waziri Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa jamii kutonyamazia matukio ya ukatili wa kijinsia na badala yake watoe taarifa za wahusika wa matikio hayo ili wachukuliwe hatua stahiki.

“Tunajitahidi kudhibiti kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kisheria na kuimarisha utoaji elimu kwa Watoto na Wanawake , ni muhimu sana jamii zetu zikaona umuhimu wa kukaa na Watoto na Wanawake kuboresha madawati ya kijinsia ili kutokomeza ukatili.” amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu baada ya Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Tanga (CCM) Mwantumu Zodo kutaka ufafanuzi kuhusu mkakati wa Serikali katika kukabiliana na ongezeko la matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, ukatili na mauaji ya Wanawake na Watoto.