Mbowe : Msiwadhalilishe wenye mawazo tofauti

0
118

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amekemea tabia ya baadhi ya vijana wa chama hicho ya kuwakosea heshima
watu ambao wanakuwa na mawazo tofauti na mawazo yao na kusema jambo hilo si la kiungwana.

Mbowe ameeleza hayo mkoani Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha Baraza kuu la chama hicho.

Amesema ni vema vijana wa CHADEMA wanaofanya vitendo hivyo wabadilike na wawe na heshima na staha hata kwa watu wanaotofautiana nao kifikra hasa wanapokutana katika mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Taifa amesema, kwa sasa chama hicho ndio chama kikuu cha upinzani nchini lakini haina maana kuwa siku zote ķitabaki katika nafasi hiyo.

Amesema unaweza ukafika muda kwa chama kingine cha siasa kuwa chama kikuu cha upinzani, hivyo hakuna maana yoyote ya kudhalilisha vyama vingine vya siasa na wanasiasa wengine.

Kikao hicho cha Baraza Kuu la CHADEMA kinahudhuriwa na Wajumbe takribani mia nne kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.