Viatu chakavu vyauzwa Mamilioni

0
107

Kampuni ya BALENCIAGA ya nchini Ufaransa ambayo ni kampuni kubwa na maarufu ya mavazi duniani imeingiza sokoni viatu vilivyotengenezwa katika muonekano wa uchakavu (distress shoes), na hivyo kuzua gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii duniani.

Bei ya viatu hivyo ambavyo vinaonekana tayari vimechakaa ama kumwagiwa taka ni kati ya dola 495 na dola 625 za Kimarekani kwa jozi moja.

Kwa pesa za Tanzania ndio tunasema viatu hivyo vinauzwa kati ya zaidi ya shilingi milioni 1.1 na zaidi ya shilingi milioni 1.4 kwa jozi moja.