Wadau sekta ya ujenzi kukutanishwa Dodoma

0
148

Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), inatarajia kuwakutanisha makandarasi na wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi, kwa lengo la kujadili mchango wao katika uchumi wa Tanzania.

Mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu isemayo Umuhimu na Mchango wa Makandarasi katika uchumi wa Tanzania utafanyika mkoani Dodoma tarehe 12 na 13 mwezi huu ukiwashirikisha wadau, waajiri, wataalamu washauri, wahandisi na wabunifu majengo.

Msajili wa CRB, Mhandisi Rhoben Nkori amesema mkutano huo wa mashauriano ambao hufanyika kila mwaka ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya ujenzi

Ametaja mada zitakazotolewa kwenye mkutano huo kuwa ni pamoja na mchango wa makandarasi katika uchumi wa Tanzania, changamoto zinazoathiri mchango wa makandarasi katika uchumi wa nchi na masuala ya kodi ya kuzingatiwa kwa makandarasi.

“Mkutano utakuwa na wadau wengi wa sekta ya ujenzi hivyo tunawakaribisha watu binafsi na mashirika kuja kuonesha bidhaa walizonazo kwa washiriki wa mkutano huu wa mwaka,” amesisitiza Mhandisi Nkori